September 11, 2016

Kufuatia kifo cha kocha wa zamani wa Simba, James Siang’a ambaye alifariki jana alfajiri nyumbani kwake Bungoma nchini Kenya baada ya kuugua kwa muda mrefu. kumekuwa na simanzi zito kwa wadau wa soka wa Kenya na Tanzania.

Siang’a ni mmoja wa makocha waliopata mafanio makubwa alipokuwa akiinoa Simba, pia alikuwa na heshima kubwa katika soka la Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla.

Marehemu Siang'a

Mara baada ya Ofisa wa Chama cha Kefoca, Bob Oyugi kutoa taarifa ya msiba huo, baadhi ya wachezaji waliowafhi kufundishwa na jkocha huyo ambaye aliwahi kuchezea Gor Mahia, Luo Union na timu ya taifa Kenya, Harambee Stars akiwa kipa, walitoa maoni yao na kueleza kuguswa na msiba huo.

Kikosi cha Simba cha mwanzoni mwa miaka ya 2000.
 
Akimzungumzia kocha huyo ambaye pia aliwahi kuwa kocha wa Moro United ya Tanzania na Express ya Uganda, kiungo wa zamani wa Simba, Shekhan Rashid alisema ni pigo kubwa kwa kuwa Siang’a alikuwa na umuhimu mkubwa katika soka la Tanzania.


“Nakumbuka alikuwa akiniheshimu na kunipa sifa ya kuwa fundi, kuna kipindi nilikuwa sipati nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza lakini kuna siku tulitakiwa kucheza na Ismailia, akaniambia nitaanza katika mchezo huo.


“Sababu ya kunianzisha aliniambia mimi ni fundi na kwa kuwa Ismailia ina mafundi wengi ni vizuri fundi akacheza na mafundi wenzake.
Matola

Shekhan


“Nakumbuka hata katika mechi nyingi dhidi ya Mtibwa Sugar alikuwa akinipanga kuanza kwa kuwa kipindi kile aliamini Mtibwa ina wacheaji wengi mafundi.


“Hakika dunia itamkubuka kwa mchango wake katika soka,” alisema Shekhan.

Naye kiungo mwingine wa zamani wa Simba, Selemani Matola alisema Afrika yote imepata pigo kwa kuwa mchango wa Siang’a ulisaidia wachezaji wengi wa Afrika na siyo wa Kenya na Tanzania tu.

Siang’a aliidakia Kenya katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1972 na pia alikuwa kocha wa Harambee Stars mwaka 1999 na 2000, kabla ya kuhamia Tanzania kufundisha Simba, Mtibwa Sugar, Moro United na timu ya taifa ya Bara kwa muda mfupi mwaka 2002.

Akiwa Simba, Siang’a aliipa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati visiwani Zanzibar mwaka 2002.

Akiwa na Moro United Oktoba 2004 Siang’a aliombwa kuinoa Taifa Stars lakini alikataa. Siang’a pia aliinoa Mtibwa Sugar kabla ya kurejea Kenya kuifundisha timu ya Gor Mahia.

Siang’a ndiye aliyeiwezeha Simba kuitoa Zamalek ya Misri waliokuwa mabingwa wa Afrika katika hatua ya 16 Bora na kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baadhi ya wachezaji wa zamani wa Simba waliofundishwa na Sinag’a ni Primus Kasonzo, Christopher Alex, Shekhan Rashid, Ulimboka Mwakingwe, Said Swedi, Ramazani Wasso, Boniface Pawasa, Victor Costa, Lubigisa Madata, Athumani Machuppa, Seleman Matola na Emmanuel Gabriel.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV