September 12, 2016

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, jana alifanya ziara ya kushtukiza kwenye Uwanja wa Uhuru baada ya kusikia malalamiko kadhaa juu ya uwanja huo ikiwemo suala la vyoo.

Waziri Nape alisikiliza malalamiko ya baadhi ya wadau juu ya uwanja huo ambao umezinduliwa hivi karibuni pia alipata nafasi ya kupiga nao picha.
 
Aliondoka uwanjani hapo na kuwaahidi kuyafanyia kazi yale yote ambayo walimjulisha.

Uwanja wa Uhuru ulifungwa kwa takribani miaka mitatu ukawa hautumiki kutokana na kuwa kwenye maboresho ikiwemo sehemu za jukwaani na kwenye nyasi za kucheza 'pitch', umeanza kutumika tangu wiki iliyopita kwa mechi za Ligi Kuu Bara kuchezwa uwanjani hapo, hiyo ikiwa ni baada ya wakandarasi kuukabidhi kwa serikali. 

 0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV