September 16, 2016

Ronaldo & Rihanna
Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anajulikana na anatajwa kuwa ndiye mwanamichezo ambaye ana wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii lakini tofauti na hapo katika fani nyingine pia anawafunika akiwa amesaliwa na mtu mmoja tu.

Mreno huyo ambaye anajulikana kwa kupenda kupendeza ana jumla ya wafuasi milioni 238 katika kurasa zake kwenye mitandao ya Facebook, Twitter na Instagram. staa pekee ambaye hajamfikia ni mwanamuziki Taylor Swift ambaye ana wafuasi milioni 246.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Taasisi ya Hispania kutoka jinni la Madridi inayojulikana kwa jina la Apple Tree Communications.Ronaldo amewazidi mastaa wengi wa fani nyingine wakiwemo Katy Perry, Selena Gomez na Rihanna ambao wana wafuasi milioni 219, milioni 205 na milioni 190.

Utafiti huo unaonyesha kuwa asilimia kubwa ya wafuasi ni wanawake wenye mri wa kati hasa kutoka Marekani.


Taylor Swift & Ronaldo

Februari, mwaka huu Ronaldo ndipo alipoanza kusika rekodi ya kuwa mwanamichezo aliyefikisha wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii kwa kusikisha milioni 200, baada ya hapo amekuwa akiongeza idadi.

Kwa sasa Ronaldo anawazidi wanamichezo wengine mastaa akiwemo mpinzani wake kutoka Barcelona, Lionel Messi na wachezaji nyota wa kikapu, LeBron James, Michael Jordan, Kobe Bryant, Kevin Durant na Steph Curry.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV