September 26, 2016


MO Bejaia ina matumaini makubwa ya kubeba Kombe la Shirikisho itakapokutana na TP Mazembe katika fainali.

Timu zote mbili zimetokea katika kundi walilokuwemo Yanga ya Tanzania ambayo ilishindwa kuvuka kwenda nusu fainali.

Mohamed Sabah, mmoja wa wataalamu wa masuala ya ufundi, amesema Bejaia wako vizuri zaidi.

“Bejaia kwa sasa wana kikosi bora zaidi. Kikubwa tunahitaji ni kufunga bao la mapema na kushinda mechi ya kwanza,” alsiema Sabah alipozungumza na mtandao wa Kingfut.

Sabah amesema, anaamini Mazembe ni timu bora. Lakini nafasi ipo kwa Bejaia ambayo hata kufika kwake fainali, kumewashangaza wengi.

Bejaia itaanzia nyumba Oktoba 28 na mechi ya pili itakuwa ni Novemba 4 mjini Lubumbashi, DR Congo.

Hata hivyo, Sabah anasisitiza kama Bejaia itashinda mechi ya kwanza. Ina uhakika wa kufanya vema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV