September 26, 2016



Mshambuliaji Mbwana Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk amefikisha mabao sita ukijumlisha yale ya Ligi Kuu ya Ubeligiji pamoja na mechi za Europa.

Katika mabao hayo sita, mawili ni ya Europa na manne ni ya ligi lakini inaonekan Samatta ni hatari zaidi katika dakika za mwisho.

Kwani katika mabao hayo sita, ni bao moja tu dhidi ya Oostende katika mechi iliyochezwa Julai 31, ndiyo alifunga katika dakika ya 10.

Lakini mabao mengine yote, amefunga kuanzia dakika ya 73 hadi 80, hali inayoonyesha kuwa kila dakika 20 za mwisho, ni mtu wa kuchungwa kweli.

Mabao aliyofunga katika mechi za Europa ni dhidi ya NK Lokomotiva, alifunga katika dakika ya 83 na mechi ikaisha kwa sare ya mabao 2-2. Mechi ya pili dhidi ya timu hiyo, akafunga pia katika dakika ya 80.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic