September 26, 2016

PLUIJM

Kiocha wa Yanga, Hans van der Pluijm ana imani na kambi ya Pemba itarekebisha mambo.

Yanga imepoteza mechi yake iliyopita ya Ligi Kuu Bara kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Stand.
Awali, Yanga ilitangaza ingeweza kuweka kambi Mwanza, lakini baadaye benchi la ufundi liliamua kikosi kirejee Pemba.

“Pemba kuna utulivu na nafasi nzuri, tunaweza kufanya mambo yetu vizuri na kutafakari.

“Kuna vitu vya kurekebisha kabla ya kurejea tena kwenye ligi. Mechi inakuja ni dhidi ya Simba, lakini tuna imani kubwa ya kurejea.

“Tutakuwa na muda, hata kama si mrefu sana, lakini tutafanya kila jambo kulingana na muda,” alisema.

Yanga imeifunga Simba mara mbili msimu uliopita ikitokea katika kambi ya Pemba.


Wachama wa Yanga kisiwani Pemba, pia wamekuwa wakisifika kwa ushirikiano mzuri wakati timu inapokuwa kambini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV