September 26, 2016

Beki wa kulia wa Paris St Germain, Serge Aurier ambaye ni raia wa Ivory Coast amehukumiwa kwenda jela miezi miwili kutokana na kukutwa na kosa la kumfanyia fujo askari polisi nchini Ufarasa.
Aurier(kushoto) siku PSG ilipocheza na Arsenal.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 23 alifanya kosa hilo jijini Paris, Mei 30, mwaka huu ambapo inaelezwa alimshambulia na kumtolea maneno makali.
AurierMbali na adhabu hiyo pia amepigwa faini ya euro 600 na mahakama na zinaweza kuongezeka euro 1,500.

Mwanasheria wa mchezaji huyo amesema atakata rufaa kupinga adhabu hiyo, lakini bado kanuni zinamruhusu kuibadili na kuifanya kuwa adhabu ya kuitumikia jamii badala ya kwenda jela.


Pia mchezaji huyo anatarajiwa kuwemo katika kikosi cha PSG kitakachocheza keshokutwa Jumatano katika Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Ludogorets.

Mpaka sasa ameshaichezea PSG mechi 5 msimu huu na kutoa asisti kwa Edinson Cavani katika mechi dhidi ya Arsenal, wiki mbili zilizopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV