September 26, 2016

Baada ya kuwa na mwanzo mzuri wa msimu wa 2016/17, Manchester City imepata pigo la kwanza baada ya kiungo wake, Kevin de Bruyne ambaye amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu kutarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne.


Kocha wa Man City, Pep Guardiola alisisitiza kuwa wanaweza kuendelea kufanya vizuri bila ya mchezaji wao huyo ambaye anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja. 







De Bruyne ambaye ni kiungo mshambuliaji aliumia katika mechi ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Swansea City, katika Premier League na kutolewa katika dakika ya 81 kwenye Uwanja wa Liberty, nafasi yake ikachukuliwa na Jesus Navas.



Tayari Guardiola alithibitisha kuwa watamkosa mchezaji huyo kuanzia mechi ya keshokutwa Jumatano dhidi ya Celtic katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic