September 26, 2016


Kocha Kalimangonga 'Kally' Ongala rasmi amerejea kuifundisha Majimaji ya Songea baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Ongala, mshambuliaji nyota wa zamani wa Yanga, amesaini rasmi leo mkataba huo kabla ya kuanza kazi Majimaji.Msimu uliopita, Ongala mtoto wa mwanamuziki marehemu Remmy Ramazani Ongala, ndiye aliyeisaidia Majimaji kubaki Ligi Kuu Bara kwa kuonyesha soka safi mwishoni mwa msimu.

Lakini Majimaji imeanza msimu huu kwa kusuasua na tayari imepoteza mechi zote, jambo ambalo limewalazimu wadhamini wake wapya, kuhakikisha wanamrejesha Ongala aliyechipukia kisoka katika timu ya Abajalo FC ya Sinza, maarufu kama Mnyama Mkubwa.

Mechi yake ya mwisho ya Ligi Kuu Bara, Majimaji imepokea kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi, Simba.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV