September 30, 2016


Ndege ya mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo imepata ajali mjini Barcelona, Hispania.

Ndege hiyo imepata ajali kwa kuteleza hadi kukwama kwenye majani na imeelezwa sababu ya ajali hiyo ni kuvunjika kwa gia ambayo hutumika wakati wa kutoa.

Ronaldo hakuwa katika ndege hiyo wakati ikitua Barcelona na kupata ajali hiyo, ila imeelezwa, tatizo hilo la gia ndiyo limekuwa chanzo.


Hakukuwa na taarifa za majeruhi na ndege hiyo haikuumia zaidi ya kukwama kwenye majani ingawa imeelezwa matengenezo yake, bado yatakuwa na gharama za juu.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV