September 5, 2016

UDOM
Gavana wa jimbo la Akwa Ibom Udom Emmanuel amesema Taifa Stars imemfurahisha kwa kuonyesha soka safi hadi amechukua uamuzi wa kutoa dola 10,000 (zaidi ya Sh milioni 21).

Pamoja na Taifa Stars kufungwa, gavana huyo alitoa kiasi hicho kwa Taifa Stars, huku akiipa Nigeria dola 25,000, zaidi ya mara mbili ya fedha walizopewa Stars.

“Ni timu yenye wachezaji wengi vijana, lakini walionyesha soka safi na la kuvutia.

“Uchezaji wa ushindani wa Tanzania ndiyo umechangia kwa kiasi kikubwa mechi ile kuwa burudani bora,” alisema.

Kipa Aishi Manula alikuwa nyota wa mchezo katika mechi hiyo ambayo, Stars ilifungwa kwa bao 1-0 lakini ilionyesha soka la ushindani na kuwatoa jasho kweli wenyeji wake.


Tayari timu zote mbili zilikuwa zimetolewa kwenye mbio za kuwania kufuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV