September 16, 2016

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amedai kuwa wao Simba wapo tayari kupewa ruhusa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwamba kikosi hicho kichezeshwe michezo miwili kwenye ratiba yao kutokana na upana wa wachezaji walionao katika msimu huu.
 Akizungumza na Championi Ijumaa, Mayanja alisema wanaomba hivyo kwa ajili ya kuwapa nafasi wachezaji wanaokaa benchi na jukwaani nao kuonyesha sehemu ya uwezo wao.

“Kama inawezekana sisi tuchezeshwe mechi mbili yaani moja hapa Dar na nyingine mkoani kwa ajili ya kuwapa nafasi wale wasiocheza na wanaokaa benchi nao kuonyesha viwango vyao.

“Wakikubali sisi wala hatuna hofu kwa sababu tuna kikosi kikubwa ambacho kinaweza kutimiza jambo hilo na bila kupata tatizo kwenye timu yoyote ile,” alisema Mayanja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV