September 26, 2016


MBEYA CITY YA MSIMU ULIOPITA
NI kama utani lakini ndiyo ukweli, Kocha wa Mbeya City, Kinnah Phiri amesema moja ya sababu ambazo zimechangia timu hiyo kufanya vibaya kwenye mchezo wa juzi Jummoasi dhidi ya JKT Ruvu, ni ufupi wa wachezaji alionao, hivyo hushindwa kubadili mfumo kulingana na mazingira ya uwanja na mchezo wenyewe.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mlandizi, Mbeya ilikubali kichapo cha mabao 2-0 yaliyofungwa na Atupele Green (penalti) na Samuel Kamuntu, kichapo ambacho Phiri anaamini mbali na makosa yao wenyewe, pia ubovu wa uwanja ulichangia.

Mmalawi huyo alisema falsafa yake ni soka la pasi nyingi na fupi, lakini ilibuma siku hiyo kutokana na ubovu wa kiwanja cha Mlandizi lakini akashindwa kujaribu mfumo wa pasi ndefu kutokana na kutokuwepo hata mchezaji mmoja mrefu kikosini mwake.

“Falsafa yetu ni pasi za chini, ndiyo maana tunapokuwa kwenye uwanja mzuri, nadra sana tukazidiwa mchezo, Uwanja wa Mlandizi si mzuri, tuliujaribu ikashindikana.

“Ningeweza kujaribu mfumo wa mipira mirefu ambao pia ndiyo mfumo wangu, lakini tatizo kikosi kizima hakuna mchezaji ‘type’ ya John Bocco, wote ni wadogo na wafupi.

 Unapotaka kucheza mfumo huu lazima uwe na mtu kama Bocco, jambo ambalo naona litatuumiza hata kwenye viwanja vingine sampuli ya Mlandizi,” alisema kocha huyo wa zamani wa Free States ya Sauz.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic