September 26, 2016Wakati zikiwa zimebaki siku nne pekee kabla ya mechi ya watani Simba na Yanga kupigwa, mshambuliaji wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo, ameweka bayana yeye hatachonga sana kuhusu mchezo huo utakavyokuwa, bali anaelekeza akili na makali yake uwanjani.

Mavugo aliyeifungia Simba mabao matatu mpaka sasa, kwa mara ya kwanza anatarajia kuiongoza timu yake hiyo kuvaana na Yanga katika mchezo wa ‘derby’ ya Dar utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Oktoba Mosi, mwaka huu.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Vital’O ya Burundi, amesema licha ya presha ya mchezo huo inavyozidi kupanda lakini kwa upande wake hataki kuzungumzia lolote kuhusiana na wapinzani wao, bali atawaonyesha watakapokutana uwanjani.

“Siwezi kusema sana juu ya mechi dhidi ya Yanga itakavyokuwa kwa sababu mimi siyo mzungumzaji mno ila nitakachokifanya ni kutenda uwanjani kama ninavyofanya kwenye mechi nyingine za timu yangu.

“Mechi itakavyokuwa vyovyote kwangu sawa kwa sababu nipo tayari na nimejiandaa kucheza na sina wasiwasi ila kwa wale ambao watataka kuona nitafanya nini basi waje kuona uwanjani na siyo kuanza kuongea sana kabla mechi yenyewe haijachezwa,” alisema Mavugo anayetumia jezi namba 11 katika kikosi hicho.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV