September 3, 2016Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,  ameiangalia timu hiyo kwa umakini na kisha kutoa onyo kwa wachezaji wenzake kutokana na hali inayoendelea kwa sasa ndani ya kikosi hicho.

Cannavaro ameanza kwa kueleza kuwa, Ligi Kuu Bara msimu huu iliyoanza wiki mbili zilizopita ipo tofauti na ushindani wa ligi za misimu ya nyuma.

Beki huyo anamaanisha kuwa, ligi ya sasa ushindani umeongezeka zaidi na kama wachezaji wenzake wataendeleza masihara, basi wanaweza wasifanye lolote msimu huu.

Cannavaro alisema licha ya ushindi wa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza dhidi ya African Lyon, bado wanahitaji kubadilika kama kweli wanahitaji mafanikio msimu huu.

“Nimefurahi tumeshinda mechi ya kwanza na Lyon lakini ukiangalia tulibebwa na ugeni wa Lyon kwenye ligi na ile ‘experience’ ya mechi nyingi za kimataifa tulizocheza lakini kama Lyon ingekuwa makini siku ile, tungepata shida sana.

“Kuhusu kikosi, wala hakina tatizo, tumekamilika vizuri tu, lakini tatizo ni masihara na kujiamini kwingi, mechi ya Ngao ya Jamii tuliyocheza na Azam hatukupaswa kuipoteza.

“Lakini kimasihara tukafungwa, sasa kama tutaendelea hivi, sidhani kama tutafanikiwa msimu huu na ukitazama ligi ya sasa ni ngumu."

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV