September 6, 2016


Kikosi cha Azam FC chini ya Kocha Zeben Hernandez raia wa Hispania kimeendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Sokoine kabla ya mechi ya kesho dhidi ya Prisons mjini Mbeya.

Azam FC watakuwa wageni wa Prisons kesho na tayari msemaji wao, Jaaffar Iddi Maganga amesema uwanja huo si mbaya sana.

“Wamejitahidi sana ukiangalia viwanja vingi vya mkoanini. Hivyo tunaamini utakuwa mchezo mzuri na mkali,” alisema.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV