September 6, 2016

BWIRE

Wakati mwingine unaweza kusema Masau Bwire bana, anaudhi kweli! Eti amesema, Simba wa sasa, hata kwa kiboko unamfukuza tu.

Masau amesema hayo akimaanisha kwamba mechi yao ya kesho dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, itakuwa laini sana.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Masau ambaye ni msemaji wa Ruvu Shooting, amesema wao watakuwa wa kwanza kuifunga Simba msimu huu.

“Tutawafunga na kuwaonyesha watu inawezekana kabisa. Zile sifa wanazowapa ni hisia tu za kuamini bila ya vitendo.

“Simba wa sasa hana makali hata kidogo, ukiwa na fimbo au watu wanaita kiboko, basi ni rahisi tu kumfukuza hata kule porini,” alisema Masau ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi kitaaluma.
Wachezaji nane wa Shooting walibaki kambini Kibaha wakati timu hiyo iliposafiri kwenda Mbeya.


Sasa wameungana na wenzao kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Simba, kesho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV