September 8, 2016

Katika kuonyesha Simba ya sasa ni mwendo wa kijeshi zaidi, licha ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting juzi Jumatano, leo Alhamisi kikosi hicho kiliendelea na mazoezi kama kawaida, lakini kocha Joseph Omog akionekana kukazia zaidi safu ya ushambuliaji.  

Kabla na baada ya mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Omog alisisitiza kuamua kuvalia njuga zaidi safu ya mbele ambayo juzi ilikosa mabao mengi ya wazi ikiongozwa na Laudit Mavugo.


Mazoezini baada ya program ya kunyoosha misuli, Omog aligawanya vikosi viwili ambapo tageti kuu ilikuwa ni jinsi ya gani mafowadi wafunge mabao kwa kupokea mipira ya krosi, pasi za kupenyezea na jinsi ya kujipanga katika nafasi zao.


Fredric Blagnon, Ame Ally ‘Zungu’ Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo ndiyo walipewa jukumu hilo huku kila aliyekosea kujipanga, Mcameroon huyo alionekana kuwa mkali zaidi.


“Kama tungekuwa makini, mechi ya jana (juzi) tungefunga hata zaidi ya mabao matano. Mavugo alipata nafasi nyingi lakini akakosa umakini, ndiyo maana nimeamua kulifanyia kazi kabla ya kitu kingine,” alisema Mcameroon huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV