September 8, 2016

Kiungo wa zamani wa Arsenal, Mathieu Flamini amejiunga na Klabu ya Crystal Palace akiwa mchezaji huru. 


  Flamini ambaye alitwaa mataji matatu ya FA akiwa na Arsenal alipokuwa akionekana ni mzuri kwenye kiungo cha ukabaji, pamoja na ubingwa wa Serie A alipokuwa AC Milan, amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja utakaomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Flamini aliondoka Arsenal baada ya kucheza mechi 246 katika awamu mbili, anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na Palace msimu huu.


Wengine waliosajiliwa na Palace msimu huu ni Andros Townsend, Steve Mandanda, James Tomkins na Christian Benteke huku Loic Remy wa Chelsea akitua kwa mkopo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic