September 16, 2016

Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime atarejea Manungu, wikiendi hii kuumana na timu yake aliyoinoa msimu uliopita, Mtibwa Sugar huku akitamba kuwa hana ujamaa na ataisambaratisha.

Tangu aihame timu hiyo inayonolewa na Salum Mayanga kwa sasa, Maxime anatarajia kukutana nayo kwa mara ya kwanza katika mechi ya kesho Jumamosi itakayopigwa Manungu Complex, Morogoro.

Mechi hiyo pia inatarajiwa kuwa kali kutokana na timu zote kufungana kwa pointi sita baada ya michezo yao minne ya awali. Kagera ipo nafasi ya nane na Mtibwa ya tisa zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.  Akizungumza na Championi Ijumaa, Maxime alisema: "Mtibwa ilikuwa msimu uliopita na huu ni msimu mpya nipo na timu nyingine na ukiangalia tumejiandaa kwa ajili ya ligi, kwa hiyo hatuangalii tunakutana na nani, yeyote tutakayekutana naye bila kujali ni nani, nia ni ushindi.

“Ishu ya kusema wachezaji wa Mtibwa wanazifahamu mbinu zangu hiyo haiwezi kuleta shida kwa sababu makocha wanahama kila siku na wanaendelea kufanikiwa hata wanapokutana na timu zao za zamani, ni ishu ya ufundi tu na wachezaji ulionao,” alisema Maxime.

Katika mechi hiyo, Maxime atatengeneza historia mpya katika maisha yake ya soka kwa kupambana na Mtibwa kwa mara ya kwanza baada ya kuitumikia kama mchezaji na baadaye kocha wa timu hiyo kwa muda wa miaka 20.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV