September 16, 2016

Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2016/2017 inatarajiwa kuendelea Jumamosi na Jumapili hii lakini kuna mabadiliko ya mchezo mmoja uliotakiwa kuchezwa Jumapili sasa utachezwa Jumanne. Mabadiliko hayo ni mwendelezo wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufanya mabadiliko kadhaa tangu kuanza kwa msimu huu.

Mchezo ambao umebadilishwa ratiba ni wa African Lyon dhidi ya Toto African ambao utakiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar, Jumapili, sasa utachezwa Jumanne Septemba 20, 2016. 

Azam FC Vs Simba zitaumana Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru

Michezo mingine ya Jumamosi itaendelea kama kawaida, Mwadui FC itakuwa mwenyeji wa Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kambarage. Mwadui ambayo inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Stand United wakati Yanga ina makali ya kuilaza Majimaji ya Songea mabao 3-0.

Mechi nyingine yenye mvuto ni kati ya Tanzania Prisons kuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wakati Azam ambayo inaongoza ligi sawa Simba kwa kuwa zina pointi sawa, zitakutana kwenye Uwanja wa Uhuru. Simba na Azam zina pointi 10 kila moja baada ya kucheza mechi nne ambako kila moja imeshinda mechi tatu na kutoka sare mmoja.


Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura
Mtibwa Sugar na Kagera Sugar zinatarajiwa kukutana kwenye Uwanja wa Manungu kwenye mchezo mwingine wa Ligi Kuu. Mtibwa ambayo imetoka kulazwa na Simba, Jumapili iliyopita, Kagera inakwenda ugenini Morogoro ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare tasa na Ndanda ambayo pia kesho itakuwa ugenini kucheza na Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji.

Katika mchezo mwingine wa kesho, Ruvu Shgooting itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Keshokutwa Stand United ya Shinyanga itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa CCM Kambarage.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV