September 16, 2016

Utamu wa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ umeendelea kuwa mtamu, hiyo ni baada ya kushuhudia wenyeji wa Daraja la Stamford wakiangukia pua kwa wageni wao ambao ni maarufu kwa jina la Majogoo.

Mabao mawili yaliyofungwa na Dejan Lovren na Jordan Henderson yameifanya Liverpool kupata ushindi dhidi ya Chelsea kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Ushindi huo umeifanya Liverpool kufikisha pointi 10 na mabao 11 ya kufunga huku ikiwa imefungwa mabao nane na kulingana pointi na Chelsea na Everton iliyo katika nafasi ya pili.

Lovren aliifungia Liverpool bao la kwanza dakika ya 17 baada ya kupokea pasi ya Philippe Coutinho na bao la pili la timu hiyo lilifungwa dakika ya 36 na nahodha Henderson aliyeuwahi mpira uliookolewa na mabeki wa Chelsea.


Kipindi cha pili Chelsea ilibadilika na kutawala mchezo ambao ilipata bao lake pekee dakika ya 61 kupitia kwa Diego Costa aliyepokea pasi ya Nemanja Matic. Katika mchezo huo beki wa Chelsea, David Luiz alichanika puani na kutibiwa baada ya kugongana na Sadio Mane wa Liverpool.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV