September 16, 2016

Mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, Samuel Eto'o ambaye kwa sasa ni kocha mchezaji wa timu ya Antalyaspor ya Uturuki amemzungumzia mchezaji mwenzake wa zamani wa Xavi Hernandez katika njia ambayo inaonyesha ni dongo kwa staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ‘CR7’.

Hivi karibuni, Xavi alinukuliwa akisema anaukubali uwezo wa Ronaldo lakini anamwonea huruma mchezaji huyo kwa kuwa anashindwa kutajwa kuwa bora kwa kuwa anacheza katika zama za Lionel Messi wa Barcelona ambaye ndiye mchezaji bora wa muda wote katika soka.

Eto'o (kushoto) na Ronaldo

Messi, Eto'o na Henry

Akijibu maoni hayo ya Xavi, Ronaldo alionyesha kuwa na hasira na kusema kuwa yeye ameshinda tuzo tatu za Ballon d'Or wakati Xavi hana tuzo hata moja.

Eto'o amefunguka kuwa anaamini Xavi alitakiwa kushinda tuzo za Ballon d'Or mara nyingi tu kama kungekuwa na haki kwa wanaotakiwa kupewa. Kauli ambayo inaonyesha dalili kuwa upinzani wa Barcelona na Real Madrid unaendelea hata kama mchezaji akiondoka kwenye timu hizo.

"Kama Ballon d'Or zingekuwa zinatolewa kwa haki, Xavi angeshinda mara tano au sita," alisema Eto'o na kuongeza: "Xavi anastahili heshima duniani kote.

"Mchezaji akishinda tuzo (Ballons d'Or) ndiyo umuone ni bora kuliko wengine siyo sawa, binafsi siku zote nitamkubali Messi kutokana na kile nilichokiona akikifanya.


"Hiyo haimaanishi kuwa Cristiano ameweka historia katika soka lakini kwangu Messi ndiyo bora."

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV