September 20, 2016


Real Madrid ambao wamekuwa na mwanzo wa asilimia 100 katika mechi zao nne za mwanzo za La Liga, sasa wanajiandaa dhidi ya Manyambizi, Villarreal.

Mechi itapigwa Jumatano, Madrid wakiwa ugenini na wanaonekana wanajua ugumu wake.

Hata hivyo katika mazoezi yao kwenye eneo la Ciudad Madrid, wachezaji wa kikosi hicho chini ya Kocha Zinedine Zidane, walionekana ni wenye furaha muda wote.

Lakini Cristiano Ronaldo na Gareth Bale walionekana kuwa vizuri zaidi hasa katika suala la kasi.


Villarreal, imekuwa moja ya timu zinazoipa wakati mgumu Madrid kila zinapokutana.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV