September 20, 2016


Kikosi cha FC Barcelona kimeendelea na mazoezi yake kwenye Chuo cha La Masia wakijiandaa na mechi yao ya La Liga dhidi ya Atletico Madrid.

Mechi hiyo itakuwa Jumatano kwenye Uwanja wa Camp Nou jijini Barcelona.

Wachezaji wa Barcelona, wakiwemo vinara wa ufungaji, Lionel Messi, Neymar na Luis Suarez maarufu kama MSN nao walionekana wako tayari.

Hiyo itakuwa ni mechi ya tano kwa kila timu katika La Liga msimu huu, huku Barcelona tayari wakiwa wamepoteza mechi moja dhidi ya Alaves ambao wamepanda daraja msimu huu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV