September 27, 2016Mshambuliaji Elius Maguri ameanza kuonyesha cheche zake nchini Oman baada ya kuisaidia timu yake ya Dhofar kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Al Suwaiq.

Maguri alifunga bao la pili katika dakika ya 73 baada ya kumegewa pande safi wakati timu yake ikiwa tayari inaongozwa kwa bao moja lililofungwa na Salim Mohamed katika dakika ya 24 kwa mkwaju wa penalti.


Maguri amejiunga na timu hiyo msimu huu na katika mechi za kirafiki tayari alianza kuonyesha cheche zake kwa kufunga mabao kadhaa kabla ya kuanza kufunga kwenye ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV