September 14, 2016


Licha ya Barcelona kuitandika Celtic mabao 7-0 usiku wa kuakia leo, ubora wa washambuliaji watatu wa Barcelona, Lionel Messi, Neymar na Luis Suares (MSN) umerejesha makali yake na kuwa tisho kwa kile walichokifanya kwenye mchezo huo.

Takwimu kwa ufupi za mchezo huo,
Barcelona 7-0 Celtic
Pasi zilizofika:    90%-80%
Mashuti:             15-3
Nafasi zilizotengenezwa: 12-0
Umiliki mpira:      65%-35%


Ikiwa ni mechi yao ya kwanza tu kucheza pamoja tangu kuanza kwa msimu huu Messi amefunga mabao 3 na kutoa asisti 1, Suarez amefunga mabao mawili na kutoa asisti 1, Neymar amefunga bao 1 na kutoa asisti 4.

 Lionel Messi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga hat-tricks nyingi zaidi katika Uefa Champions League akiwa na hat-trick suta akimzidi Cristiano Ronaldo ambaye ana 5.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV