September 7, 2016
Dakika ya 90 + 5: Mwamuzi anamaliza mchezo. Matokeo ni 0-0.

Dakika ya 90 + 3: Wanapiga faulo, mabeki wa Ndanda wanaokoa.

Dakika ya 90 + 2: Yanga wanapata faulo ndani ya eneo  la lango la Ndanda.

Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 5 za nyongeza matokeo bado 0-0.

Dakika ya 89: Yanga bado mambo ni magumu kwao kwa kuwa wapinzani wao wanawapa upinzani mkali.

Dakika ya 85: Timu zote zinaanza kucheza mipira mirefu.
 
Dakika ya 80: Matokeo bado ni 0-0.

Dakika ya 75: Mchezo bado unaonekana kuwa mgumu kwa timu zote. Yanga wanashindwa kuumiliki mpira muda mwingi kwa kuwa wanapopiga pasi nyingi zinapotea au kwenda ndivyo sivyo.
 
Dakika ya 67: Mchezo ni mgumu, timu zote zinashindwa kumiliki mpira muda mrefu kwa kupigiana pasi kutokana na nyasi za uwanja kutokuwa na ubora mzuri.

Dakika ya 62: Yanga wanapata faulo nje ya eneo la 18, wanapiga mabeki wa Ndanda wanaokoa, Thaban Kamusoko anajaribu kupiga shuti linazuiliwa.

Dakika ya 59: Deus Kaseke ambaye alipata kadi ya njano kipindi cha kwanza, anatoka, anaingia Juma Abdul.

Dakika ya 56: Donald Ngoma anajaribu lakini anashindwa kuipenya ngome ya Ndanda.

Dakika ya 50: Ndanda wanaonekana kuwa wagumu kufungika, Yanga nao wanaonyesha kutokata tamaa ya kupambana.
 
Kipindi cha pili kimeanza.

Timu zinaingia kwa ajili ya kuanza kipindi cha pili.

Kipindi cha kwanza kimekamilika 

Dakika 45: Muda wowote kuanzia sasa mchezo utakuwa ni mapumziko.

Dakika ya 38: Mchezo bado ni mgumu kwa timu zote na hakuna ambayo imeona lango la mwenzake. Yanga wanamiliki mpira katikati ya uwanja lakini wanakutana na upinza ni mkali kutoka kwa Salum Telela wa Ndanda.
 
Dakika ya 35: Matokeo bado ni 0-0, hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.

Yanga wanaonekana kumiliki mpira muda mwingi lakini, wenyeji Ndanda wanakuwa wagumu kukubali kufungika.
 
Idadi ya mashabiki  iliyojitokeza kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona siyo kubwa sana.

Mchezo huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, unafanyika kwenye Uwanja wa Nangwana ambapo Yanga imeshacheza mechi moja na ina pointi tatu huku Ndanda ikiwa imeshacheza mechi mbili na zote haikupata ushindi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV