September 7, 2016


AME

Mshambuliaji wa Simba, Ame Ali, amemkera kocha wake Joseph Omog ambaye ameamua kumpumzisha kwenye programu zake.

Straika huyo aliyejiunga na Simba hivi karibuni kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Azam FC, mpaka sasa hajapewa nafasi ya kucheza kikosini hapo kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara ambazo timu hiyo imeshacheza.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema, Omog aliamua kutomjumuhisha Ame kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika juzi Jumatatu kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar kutokana na vitendo vyake hivyo.

“Ame ameonekana hana nidhamu ndani ya timu, kocha akaamua leo (juzi) asimjumuhishe kwenye mazoezi yake ya mwisho kuelekea mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting wa Jumatano (leo).

“Unajua Ame amekuwa ni mtu wa ‘excuse’ nyingi, yaani mara kwa mara amekuwa akiaga anakwenda kwao kutatua matatizo ya kifamilia, hilo limeonekana kumuudhi kocha, sasa hamtaki,” alisema mtoa taarifa huyo.

Akimzungumzia Ame, Omog amesema: “Ni muda mrefu ameniaga anakwenda kwao mke wake anaumwa, ukiangalia timu ipo kwenye maandalizi ya ligi na wale wachezaji waliokuwa timu ya taifa wote wamejiunga na timu kasoro yeye.

“Kwa sasa hana nafasi kwenye kikosi changu kwa sababu bado kiwango chake hakijaniridhisha, anatakiwa kujituma zaidi kama kweli anataka kucheza soka.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic