September 12, 2016

Klabu ya Newcastle United leo imezindua sanamu lenye taswira ya mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Alan Shearer ambaye pia anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi katika timu hiyo.

Sanamu hilo limezinduliwa nje ya Uwanja wa St James' Park ambapo gharama ya jumla ya utengenezwaji wake inatajwa kuwa ni pauni 250,000.
Shearer mwenyewe alikuwepo wakati wa uzinduzi huo akiwa pamoja na kocha wa zamani wa timu hiyo, Kevin Keegan pamoja na kocha mwingine wa zamani Terry McDermott.

Snamu hilo lenye urefu wa futi 9 lilipokelewa kwa furaha na mashabiki wa Newcastle ambayo kwa sasa inashiriki katika Championiship.

Shearer ambaye aluiwahi kukataa ofa kubwa ikiwemo ya Manchester Unted alifunga mabao 148 katika mechi 303 alizoichezea timu hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV