September 12, 2016

Beki wa kushoto anayechea katika Ligi Kuu ya England 'Premier League' akiwa ni mchezaji wa timu ya Crystal Palace, Pape Souare amejeruhiwa katika ajali mbaya ya gari alipokuwa katika mitaa ya Jiji la Londo, ambapo ksa sasa yupo hospitali akipata matibabu.

Souare, 26, ameumia kiasi na imeelezwa kuwa atakuwepo hospitalini kwa muda kabla ya kuruhusiwa.


Mchezaji huyo ambaye alikuwemo katika kikosi cha timu yake kilichocheza dhidi ya Middlesbrough, wikiendi iliyopita anaendelea vizuri.

"Klabu inaendelea na mchakato wa kufuatilia kilichotokea, tunawapa pole familia ya Pape pamojana mchezaji mwenyewe,” ilieleza taarifa ya Palace.

Beki huyo raia wa Senegal alitua klabuni hapo akitokea Lille, Januari mwaka 2015.


1 COMMENTS:

  1. Daaaaahhhh,,kwa kweel habari ya juu ni nzuri lakini mwandishi wa hiyo habari,ameandika vibaya sana,yaaan haieleweki,story ipo miguu juu kichwa chini yaani daaahh,yaan story haivutii hata kidogo kuisoma,sasa sijui mtu wa michezo ninayemuheshimu Saleh jembe,kaipitia au hajaipitia hii story kwa kweli,ni aibu kwa huyo mwandishi,hasa kwa siye pia mabao tupo katika tasnia hiyo ya habari hususani za kimichezo aina hii ya uandishi inatia aibu hasa kwa blog kubwa kama hii.Ushauri wangu kwa Saleh jitahidi kupitia story za hawa waandishi wako kabla hawaja-upload,,watakutia aibu kama hii.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV