September 12, 2016

Staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameamua kuchukua mapumziko ya mkuda mfupi kwa kujiachia na mwanaye wa kiume kisha kutupia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ronaldo akiwa amevaa miwani na wigi walionekana ni watu wenye furaha ikiwa ni muda mfupi baada ya Ronaldo kuisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao 5-2 katika La Liga dhidi ya Osasuna.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31, alikuwa nje muda mrefu kutokana na kuuguza majeraha ya mguu ambapo aliumia katika fainali ya Euro 2016.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV