September 25, 2016


Kocha wa Simba, Joseph Omog amesema baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji ya Songea, wanarejea kwenda kufanya marekebisho ya mambo kadhaa ambayo wameyaona.

Hata hivyo, amesisitiza suala la kupoteza nafasi nyingi za wazi, ni kati ya yale ambayo yatafanyiwa kazi kwa ukaribu zaidi.


“Nafasi nyingi sana tumepoteza, kama unakutana na timu iko makini zaidi ni hatari sana. Unapotengeneza, lazima ufunge.

“Hilo na mengine mengi tutayafanyia kazi kwa ajili ya mechi ijayo. Lengo letu ni kuendelea kukusanya pointi tatu,” alisema.

Mechi ijayo ni dhidi ya Yanga na itachezwa Oktoba Mosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Katika mechi dhidi ya Majimaji, Simba walipoteza nafasi nyingine za kufunga, zikiwemo zile wachezaji wake walizoshindwa kupeana pasi katika nafasi nzuri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV