September 11, 2016
FULL TIME!

Simba imepata ushindi wa mabao 2-0.
 
Dakika ya 90 + 7: Mwamuzi anapuliza kipenga kumaliza mchezo.

Dakika ya 90 + 6: Blagnon wa Simba anapata nafasi ya kufunga lakini kipa wa Mtibwa anaokoa, inakuwa kocha ambayo haikuwa na matunda.

Dakika ya 90 + 5: Mchezo unaendelea. Timu zote zinashambuliana kwa zamu.
 
Dakika ya 90: Mchezo unaendelea, mwamuzi wa akiba anajiandaa kuonyesha dakika za nyongeza.
 
Dakika ya 88: Kipa ameinuka na mchezo unaendelea.
 
Kipa wa Mtibwa, Makangana anaendelea kutibiwa uwanjani, mchezo bado umesimama.
 
Dakika ya 85: Mchezo umesimama, kipa wa Mtibwa Sugar, Abdallah Makangana ameumia wakati wa kuwania mpira langoni kwake.
 
Dakika ya 80: Simba wanatawala mchezo, kasi ya Mtibwa imepungua.
 
Dakika ya 75: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Ajib anaingia Jamal Mnyate.
 
Dakika ya 73: Mtibwa wanamtoa Ibrahim Juma, anaingia Hussein Javu.
 
Dakika ya 70: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Kazimoto anaingia Said Ndemla. Simba wanaongoza kwa mabao 2-0.
 
Mavugo amefunga bao hilo, baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Mwinyi Kazimoto, ambaye alimpatia pasi kisha Mavugo akautupia mpira wavuni.

Dakika ya 66: Mavugoooooooooo!!! Goooooo!!!

Dakika ya 64: Mchezo umeongezeka kasi.
 
Dakika 61: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Kichuya anaingia Blagnon.

Dakika ya 57: Mtibwa wanafanya mabadiliko, anatoka Kelvin Idd anaingia Mohamed Juma.
 
Dakika ya 52: Ibrahim Ajib anaipatia Simba bao la kwanza akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopiwa na Kichuya.
 
GOOOOOOOO!!! Ibrahim Ajib anafunga bao


Dakika ya 46: Kipindi cha pili kimeanza, hakuna mabadiliko kwa kila timu. Wachezaji ni walewale.

KIPINDI CHA KWANZA KIMEKAMILIKA
Hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.

Mwamuzi anapuliza kipenga kuhitimisha kipindi cha kwanza.
  
Dakika ya 45 + 2: Muda wowote mwamuzi anaweza kumpulize kipenga cha kukamilika kwa kipindi cha kwanza.

Dakika ya 45: Mtibwa wanapata kona, mwamuzi wa kaiba anaonyesha dakika mbiliza nyongeza:
 
Dakika ya 42: Idadi ya mashabiki ni wengi hasa wale wa Simba, wanaishangilia kwa nguvu timu yao.
 
Dakika ya 40: Kichuya anawatoka mabeki wa Mtibwa anaingia kwa kasi ndani anapiga krosi ambayo inaokolewa na mabeki wa Mtibwa.
 
Dakika ya 35: Kasi ya mchezo imeongezeka sasa timu zinashambuliana kwa zamu, Simba wanajibu mapigo ila Mtibwa nao wanaongeza kasi ya kushambulia.
 
Dakika ya 32: Mtibwa wanafanya shambulizi kali lakini mpira unatoka njeya lango.
 
Dakika ya 25: Mtibwa wanazidi kuelewana.
 
Dakika ya 18: Mtibwa wanaonekana kuchangamka na kuanza kuwapa presha Simba.

KIKOSI CHA MTIBWA KILICHOANZA LEO HIKI HAPA: Abdallah Makangana, Ally Sharifu, Issa Rashid, Kassian Ponera, Nditi, Silim Mbonde, Kelvin Idd, Ally Yussuph, Stamili Mbonde, Ibrahim Juma, Haruna Chanongo.

KWA KUKUKUMBUSHA TU KIKOSI CHA SIMBA KILICHOANZA LEO HIKI HAPA: 
Angaban, Bokungu, Mohamed Hussein, Lufunga, Mwanjale, Kichuya, Jonas Mkude, Mzamiru, Mavugo, Ajibu, Kazimoto.
Dakika ya 15: Mtibwa wanafanya shambulizi kipa wa Simba, anaokoa inakuwa kona.
 
Dakika ya 12: Mchezo bado haujawa na kasi kubwa, Simba wanamiliki sehemu kubwa ya mchezo, mashambulizi ni ya hapa na pale lakini siyo makali. Mchezo unachezwa zaidi katikati ya uwanja.

Dakika ya 8: Simba wanapiga pasi nyingi, uwanjani kuna dalili za mvua.


Dakika ya 5: Mchezo bado haujashika kasi, Simba wamepata kona moja lakini hakuwa na faida. 
 
Dakika ya 1: Mchezo umeanza.


Timu zimeshaingia uwanjani, mchezo huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara utaanza muda wowote kuanzia sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV