September 11, 2016

Mshambuliaji mkongwe wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amesemakuwa anaamini mshambuliaji chipukizi wa timu hiyo, Marcus Rashford atakuwa kuwa mchezaji mkubwa duniani ikiwa ataendelea kuonyesha ubora alionao sasa.

Rashford ambaye ana umri wa miaka 18 amekuwa akionyesha uwezo mzuri licha ya kuwa hana uhakika wa kuanza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. 

"Ni chipukizi ambaye ana umri wa miaka 18 tu, bao ana muda wa kuendelea kufanya vizuri na kujifunza. Nafikiri jinsi anavyoingia mchezoni unaona kabisa ni aina ya mchezaji gani.


“Kila matu anazungumzia kipaji chake na jinsi ambayo anaingia mchezoni.

"Siyo kwamba anatakiwa kuwa staa leo na kuiteka dunia lakini taratibu ataingia kwenye mfumo na kuwa mchezaji mzuri, kabu inajua hilo, kocha anajua na hata timu kwa jumla inajua juu ya hilo,” alisema Ibrahimovic alipokuwa akizungumza na kituo cha runinga cha MUTV.

"Tunajua ubora wake kwa kuwa tunamuona kila siku. Hakuna haja ya kufanya haraka kumuingia kwenye timu na kumpa presha kubwa kwa kuwa inaweza kumuathiri,” aliongeza mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV