Mwamuzi anamaliza mchezo, Yanga inaondoka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Majimaji.
Majimaji wanaonekana kukata tamaa, wanaonyesha kusubiri mchezo umalizike tu.
Dakika ya 90: Yanga wanaongoza mabao 3-0, mchezo unaweza kumalizika muda wowote kuanzia sasa.
Tambwe anaipatia Yanga bao la tatu akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Simon Msuva, ambaye aliambaa na mpira kutoka upande wa kulia.
GOOOOOOOOOOOOOO!!! TAMBWEEEEEEEE!
Dakika ya 82: Beki wa Yanga, Dante yupo chini, ameumia mguu, anatibiwa, mchezo umesimama.
Dakika ya 79: Amissi Tambwe anaipatia Yanga bao la pili baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa kutoka upande wa kulia.
GOOOOOOOOOO!!!!!!
Dakika ya 73: Kipa wa Majimaji aligongana na wachezaji wa Yanga wakati wa kuokoa, Tambwe akamalizia mpira wavuni, lakini mwamuzi anakataa kuwa siyo bao ni faulo kwenda kwa Yanga.
Dakika ya 73:Tambwe anatupia mpira wavuni, ila kipa wa Majimaji yupo chini, bado haijajulikana mwamuzi atachukua hatua gani.
Dakika ya 65: Donald Ngoma wa Yanga, anapiga shuti lakini linatoka nje ya goli.
Dakika ya 60: Mchezo unaendelea kwa timu zote kushambuliana kwa zamu.
Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Coutinho raia wa Brazil, yupo jukwaani akifuatilia mchezo huu. Coutinho alitua Dar es Salaam, Jumatano iliyopita.
Dakika ya 55: Yanga wanafanya shambulizi kali, lakini Tambwe anakosa bao baada ya mpira wa kichwa aliopiga kutoka nje/
Dakika ya 50: Majimaji wanafanya shambulizi wanapata nafasi ya wazi lakini washambuliaji wake wanakosa umakini.
Dakika ya 46: Kipindi cha pili kimeanza
Timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya kipindi cha pili.
KIPINDI CHA KWANZA KIMEKAMILIKA
Dakika 45 + 2: Mwamuzi anapuliza kipenga kumaliza kipindi cha kwanza. Timu zote zinaelekea kwenye vyumba kupumzika.
Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika mbili za nyongeza.
Dakika ya 44: Kamusoko anatawala eneo la katikati ambapo anawapitishia mipira wachezaji wanzake wa Yanga lakini wanashindwa kuzifanyia kazi vizuri.
Dakika ya 42: Mchezo umepungua kasi lakini mpira bado upo zaidi katika lango la Majimaji.
Dakika ya 38: Yanga wanafanya shambulizi kali, Tambwe na Msuva wanaelewana na kucheza vizuri lakini wanashindwa kutumia nafasi.
Kumbuka kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Yanga kuutumia Uwanja wa Uhuru ikiwa ni baada ya kufungwa kwa miaka mitatu ukifanyiwa maboresho. Simba na Ruvu Shooting ndizo timu zilizofungua dimba katika ufunguzi.
Dakika ya 35: Yanga ndiyo mbao wanaendelea kutawala mchezo ambapo mpira umekuwa ukichezwa muda mwingi kuanzia katika nusu ya eneo la Majimaji.
Dakika ya 30: Majimaji wanaonyesha kuwa na nidhamu kutokana na maamuzi yao katika kuzuia na kuuchezea mpira.
Dakika ya 28: Yanga wanafanya shambulizi kali, linapigwa shuti kali na Simon Msuva, linagonga nguzo na kurejea uwanjani lakini Majimaji wanaokoa.
Dakika ya 25: Yanga inaongoza bao 1-0, Majimaji wanawabana Yanga lakini mashambulizi yamekuwa ya kupokezana.
Yanga inaongoza bao 1-0, mfungaji wa bao hilo ni Deus Kaseke ambaye alimalizia mpira uliogonga mwamba baada ya Simon Msuva kukosa penalti.
Kikosi cha Yanga kinachocheza leo:
1. Ali Mustafa
2. Juma Abdul
3. Haji Mwinyi
4. Andrew Vicent
5. Nadir Haroub
6. Thabani Kamusoko
7. Saimoni Msuva
8.Deus Kaseke
9. Donald Ngoma
10. Amis Tambwe
11. Obrey Chirwa
Akiba:
- Beno Kakolanya
- Hassani Kessy
- Oscar Joshua
- Kelvin Yondani
- Juma Mahadhi
- Mateo Antony
- Yussuf Mhilu
Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga dhidi ya Majimaji unachezwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment