October 11, 2016


 

Bondia Mussa Hassan, maarufu kama Mgosi ameuwawa baada ya kuvamiwa na watu wanaoelezwa kuwa ni vibaka.

Kwa muhibu wa Super D Boxing, ambaye ni mmoja wa makocha maarufu wa mchezo wa ngumi nchini amesema, vibaka hao wamemvamia katika eneo la Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, na kumpiga hadi alipopoteza uhai.

“Amefariki dunia jana wakati anatoka ofisini kwake, alikuwa ana saluni,” alisema Super D.

Mipango ya mazishi inafanywa na kocha wake anaitwa Mbaruku Heri anasimamia hilo jambo kwa kushirikiana na ndugu zake.

Gongo la Mboto ni kati ya eneo hatari jijini Dar es Salaam kutokana na kuwa na vibaka wakatili ambao wamekuwa wakitoa uhai wa watu mara kwa mara kwa lengo la kuwaibia.

TUNAWAOMBA RADHI KWA PICHA HII YA CHINI. LAKINI TUNATAKA KUWAONYESHA UKATILI WA HOVYO WA WANADAMU
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV