October 10, 2016


MMACHINGA (KUSHOTO) AKIMKABIDHI TAMBWE TUZO YA UFUNGAJI BORA

Baraza la Michezo la Taifa (BMT), limeibuka na kueleza kwamba mchakato wa klabu ya Yanga kuikodisha timu yake una tatizo.

Halo hiyo imeonyesha kuwashangaza Wanayanga wengi wakiemo wale waliohudhuria mkutano uliopitisha uamuzi huo.

Wanachama hao walikutana kwenye mkutano na kulizungumzia suala hilo na mwisho wakakubaliana.

Mmoja wa wachezaji wa zamani wa Yanga, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’, amelizungumzia huku akiona BMT wamekurupuka.

“Niwe wazi kuwa hawa wamekurupuka, BMT hawakutakiwa kutoa kauli hiyo kwa wakati huu, badala yake walitakiwa kukaa chini na kulitafakari kwa kina kisha kuwaambia Yanga nini kifanyike lakini siyo kuliwahisha kiasi hiki kuibuka na kupinga mchakato.


 “Nadhani muhimu zaidi ni elimu kutolewa kwa wananchi juu ya faida za mfumo wenyewe. Naamini ni mzuri na utaisaidia klabu mbeleni.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV