October 11, 2016


Beki wa Simba, Juuko Murshid ametua mjini Mbeya tayari kuwavaa wenyeji Mbeya City, kesho.

Simba tayari ipo mjini Mbeya lakini Juuko alikuwa na majukumu ya kuitumikia timu yake ya taifa ya Uganda iliyokuwa inaivaa Ghana katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia.

“Kweli Juuko ameshatua na ameungana na wenzake na leo tutafanya naye mazoezi mepesi,” kilieleza chanzo ndani ya Simba.

Simba imekuwa ikiendelea na maandalizi yake vizuri kujiandaa kuivaa Mbeya City ambayo inaonekana kuupania mchezo huo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV