October 31, 2016

SHIZA KICHUYA

MSIMU wa Ligi Kuu Bara wa 2016-17, unaonekana kuchangamka zaidi katika suala la ufungaji wa mabao, jambo ambalo linaonyesha hali ikiendelea hivi kutakuwa na ongezeko kubwa la mabao ya kufunga.

Kabla ya mechi za jana, hadi mechi za juzi, tayari timu zilizocheza zilikuwa zimefunga mabao 196, jambo linaloonyesha timu zinaweza kumaliza mzunguko wa kwanza zikiwa na zaidi ya mabao 250.

Msimu uliopita, hadi mwisho kulikuwa na mabao 496 yaliyotikiza nyavu, hadi sasa ikionekana kukiwa na deni la mabao 300 ambayo kwa wastani yanaonekana ni machache kama wafungaji wataenda na mwendo huu.

Yanga iliweka rekodi msimu uliopita, ilifunga mabao 70 katika mechi zake 30 za Ligi Kuu Bara. Kabla ya mechi ya jana dhidi ya Mbao FC ilikuwa imepachika mabao 24 na kuendelea kuongoza.

Utaona kwa mwendo wa Yanga, inaonekana ina uwezo wa kufunga tena mabao 70 na kuendelea kuifanya idadi ya ufungaji wa mabao kuwa juu zaidi. Simba nao hadi juzi baada ya mechi yao dhidi ya Mwadui FC walikuwa wamefikisha mabao 21. Wakati hadi mwisho wa msimu uliopita walimaliza mechi 30 wakiwa na mabao 45.

Utaona Simba kabla ya nusu ya msimu, tayari wana mabao karibu nusu ya msimu uliopita, huenda wanahitaji mechi mbili kufikia au kuvuka nusu ya mwaka jana. 

Simba na Yanga, zinaenda na kasi nzuri ambayo inaweza kuvuka msimu uliopita. Lakini Azam FC ambao walishika nafasi ya pili kwa ufungaji msimu uliopita wakiwa na mabao 47, wanaonekana kusuasua kidogo. Kwani hadi sasa wana mabao 15 na wanatakiwa kuongeza kama wachangiaji bora.

Kila anayefanya vizuri, mara nyingi ni yule anayepambana kufanya bora zaidi ya jambo fulani ambalo aliwahi kulifanya kabla.

Wafungaji ambao walikuwa bora lazima wapambane kufanya bora zaidi lakini ambao hawakuwa bora kama akina Mohamed Ibrahim, Juma Mahadhi na wengine, msimu huu ndiyo wakati wao.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic