October 10, 2016

KIFARU

Kikosi cha Mtibwa Sugar kipo jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi yao dhidi ya Yanga Jumatano.

Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema, wana uhakika wataimaliza Yanga kwa kuwa wanazijua mbunu zake na inaongozwa na wachezaji wengi ambao ni wa kwao.

“Sasa wana beki Dante, lakini bado kuna wachezaji waliowahi kutokea kwetu Mtibwa. Tunajua tutapita wapi lakini Yanga kwetu ni sehemu ya kurekebishia mambo yetu hasa pointi.

“Lakini nikuambie ndugu yangu, hawa Yanga tunazijua sana mbinu zao na mara nyingi unajua tunawasumbua sana. Hivyo wala hatuna hofu hata kidogo,” alisema Kifaru.


Amesisitiza Mtibwa Sugar ambayo ipo katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 12 wakati Yanga ipo katika nafasi ya 6 na pointi 11 ingawa ina mechi moja mkononi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV