October 12, 2016



Akiwa anajiandaa kujitupa uwanjani leo kuvaana na Mtibwa Sugar, Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, ametamba kuwa atatumia mbinu za Simba kuwamaliza vijana hao wa Morogoro.

Yanga inatarajiwa kuvaana na Mtibwa katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo jioni.

Katika mechi hiyo, Yanga itaingia uwanjani ikiwa na hasira ya kuzikosa pointi za mchezo uliopita dhidi ya Simba baada ya kushindwa kulinda bao lao moja walilokuwa wanaongoza kabla ya Shiza Kichuya kusawazisha dakika ya 87 na mechi kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Pluijm alisema Mtibwa siyo timu ya kuibeza kutokana na aina yao ya uchezaji ya kutumia nguvu na kulinda lango lao.

Pluijm alisema, katika mechi hiyo, ataingia kwa tahadhari huku wakihofia kupata majeraha na kikubwa watacheza soka la kushambulia dakika zote 90, lakini pia akikiri kuwa aliwaangalia walipofungwa na Simba mabao 2-0 na kwenye ligi na kugundua udhaifu wao.

 “Maandalizi haya niliyoyafanya kwenye kikosi changu, yanatosha kabisa kupata matokeo mazuri ya ushindi ili tujiwekee mazingira mazuri ya kuutetea ubingwa wetu.

“Katika mechi hiyo, tutaingia uwanjani tukiwa tayari tumeshawajua wapinzani wetu Mtibwa baada ya kuwaona mechi dhidi ya Simba, siyo timu mbaya, ipo vizuri sana.


“Baada ya kuwaona, nimeona sehemu zenye upungufu kwenye kikosi changu ambazo zinahitajika kuboreshwa ili tusiwape nafasi ya kumiliki mpira Mtibwa, hivyo ni matarajio yangu katika mechi hiyo kuibuka na ushindi,” alisema Pluijm.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic