October 1, 2016


MKURUGENZI MKUU WA MULTICHOICE TANZANIA, MAHARAGE CHANDE (WA TATU KULIA) AKIMSILIZA MMOJA WA WASIOONA WAKATI WA HAFLA HIYO FUPI MBELE YA WAANDISHI WA HABARI.
Kampuni ya Multichoice Tanzania imekabidhi vifaa maalum vya michezo kwa watu wasioona kwa ajili ya ushiriki wao wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya fimbo nyeupe Oktoba 6, mwaka huu jijini Mbeya.

Lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuhamasisha jamii na watumiaji wa barabara, kuiheshimu fimbo nyeupe na kumsaidia mtu asiyeona anapotembea barabarani.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande alisema: “Tuna furaha kubwa kushirikiana na ndugu zetu wasioona wa Dar es Salaam katika kuwaandaa kushiriki maadhimisho yatakayofanyika Mbeya.

“Tutaendelea kuwa mstari wa mbele kushirikiana na jamii yetu kila fursa inapojitokeza”.

Vifaa vilivyotolewa ni mipira minne ya goalball, domino set nne, karata nne, fedha za nauli na kujikimu kwa timu hiyo ya wasioona. Mchango huo wa Multichoice una thamani ya Sh milioni 3.1.


MultiChoice Tanzania ni miongoni mwa kampuni za huduma ya ving’amuzi ikitumia king’amuzi cha DStv ambacho kina burudani za michezo na filamu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic