October 30, 2016Simba imezidi kujikita kileleni baada ya kuitwanga MWadui FC kwa mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, jana.

Pamoja na hivyo, Kocha wa Simba, Joseph Omog amesisitiza kuwa lazima kikosi chake kihakikishe kinashinda mabao zaidi ingawa suala la viwanja vya mikoani ni tatizo.

"Viwanja vya mikoani ni tatizo kwa kweli, unaona ni kiwango duni na inakuwa ni tatizo kwa wachezaji na afya yao.

"Lakini bado tunatakiwa kushinda mabao zaidi hasa kwa kuwa nafasi tunazipata, lazima kuzitumia," alisema.

"Soka ni mchezo wenye makosa, mnatakiwa kuendelea kujifunza kila siku. Tunaendelea kurekebisha jambo kila baada ya mechi moja."

Simba ilishinda tatu, mabao mawili yakifungwa na Mohammed Ibrahim na moja likifungwa na Shiza Kichuya.


Lakini Simba ilipoteza zaidi ya nafasi mbili safi kabisa za kufunga kupitia kwa Laudit Mavugo na Muzamiru Yassin.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV