October 30, 2016


Beki kisiki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani atakaa jukwani wakati Yanga inaivaa Mbao FC kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Yondani ni majeruhi na tatizo ni mguu wake. Juzi alipumzishwa mazoezi, jana pia hakufanya.

Lakini leo Yanga wamethibitisha kuwa Pluijm ameona apumzike ili kurejea katika hali yake kabisa.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wanashuka dimbani leo katika mechi yake ya 12, tayari wakiwa wamekusanya pointi 24.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV