October 30, 2016


Baada ya kurejea, Kocha Hand van der Pluijm amesema hata mechi dhidi ya Mbao FC leo, pia itakuwa ngumu kwao.

Pluijm raia wa Uholanzi aliamua kuandika barua kuachia ngazi, lakini uongozi wa Yanga ukamuangukia na kumfanya abadili uamuzi wake huo.

Leo Yanga inapambana na Mbao FC kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mechi ya kwanza baada ya Pluijm kurejea.

"Najua itakuwa mechi ngumu, timu zote zinajiandaa na inakuwa faraja kwao kushinda dhidi ya Yanga ambao ni mabingwa.

"Wachezaji wangu wako tayari na wanajua sisi ni kina nani na wanaocheza na sisi wanataka nini," alisema.

Yanga imeonyesha kurejea katika kiwango chake kwa kushinda mabao mengi katika kila mechi, ikianza na kuitandika Kagera Sugar mabao 6-2 na JKT Ruvu mabao 4-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV