October 30, 2016


Wakati bondia Mtanzania wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ akimchakaza Mchina, Chengbo Zheng katika raundi ya kwanza tu, usiku wa kuamkia jana, raia wengi wa China waishio nchini walikuwa ukumbini Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Licha ya kwamba walionyesha ushirikiano wao tokea mwanzo, lakini wako walikuwa na hofu kutokana na muonekano wa Dulla Mbabe, kwamba jamaa amejazia kweli, yaani mtu kweli.

Pamoja lilivyoanza, Wachina hao hawakupata muda wa kushangilia hata sekunde moja zaidi ya wao pia kuwa na midadi ya kukwepa makonde mfululizo ya Dulla Mbabe na mwisho Zheng akaona isiwe tabu akatulia sakafuni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic