October 26, 2016

BOSSOU
Beki wa Yanga, Vincent Bossou raia wa Togo ameweka wazi hisia zake kwamba wao hawataathiriwa na kitendo cha kujiuzulu kuinoa timu hiyo aliyekuwa kocha mkuu, Hans van Der Pluijm, badala yake wataendelea kupambana kushinda mechi zao ili kutetea ubingwa wao.

Pluijm alikacha kuifundisha Yanga hivi karibuni mara baada ya uongozi wa timu hiyo kuzungumza na Mzambia, George Lwandamina aliyetokea Klabu ya Zesco kwa ajili ya kuja kuifundisha timu hiyo.

Bossou amesema kwamba licha ya kutambua mchango wa Pluijm katika timu hiyo, ikiwemo ya kuwapa ubingwa wa ligi na Kombe la Shirikisho (FA), hayo yote hawana budi kuyasahau na kuendelea kuipigania timu hiyo zaidi kwa ajili ya kutetea mataji waliyonayo mkononi.

PLUIJM

“Hayo ni maamuzi binafsi yaliyofanywa na Pluijm na hakuna anayejua kwa nini amefanya hivyo lakini nadhani hawezi kukosa sehemu ya kwenda kufanya kazi kwa sababu ana uwezo mkubwa sana.


“Lakini pia sisi hatutakiwi kuwaza sana juu ya kuondoka kwake kwa sababu tupo kwenye ligi na tunapigania kutetea ubingwa, hivyo tunachofanya ni kuwaza mechi zetu na namna gani tutapata ushindi lakini siyo suala lake kwa sababu tayari kashaondoka,” alisema Bossou.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic