November 1, 2016Malifedha Christopher Mashali amesema mwanaye atazikwa kwa imani za dini ya Kikristo.

Bondia mahiri nchini, Thomas Mashali ameuwawa kwa kupigwa na watu wasiojulikana na kifo chake kimehusishwa na mambo mengi, ingawa hadi sasa kumekuwa hakuna uhakika.

MALIFEDHA MASHALI (WA PILI KULIA), AKIJADILI JAMBO NA KAIKE SIRAJU NA WADAU WENGINE WA MCHEZO WA NGUMI NCHINI.

Taarifa zilieleza, bondia huyo alibadili dini na kuwa mwislamu na alijulikana kwa jina la Mohammed.

Lakini baba yake amesisitiza, lazima azikwe kama mkristo na si vinginevyo.

“Sikuwa nimeonana naye siku nyingi sana, inaweza kufika miezi mitatu hivi. Lakini watu wananiambia taarifa za kwamba alibadili dini, mimi silijui hilo.

“Maana hakuwahi kuniambia, hivyo atazikwa kwa imani za Kikistro,” alisema.


Maandalizi ya mazishi yake yanaendelea na huenda, Mashali akazikwa kesho jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV