November 1, 2016Simba wamesema wako tayari kwa ajili ya mechi ya Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, kesho.

Meneja wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema vijana wake wanataka kushinda ili kuendeleza rekodi ya ushindi.

“Wote tunajua ni mechi ngumu lakini wachezaji wa Simba wanataka kushinda. Sisi tunataka kufanya vema na kama ni ubingwa tunajua utapatikana na uhakika wa pointi tatu.

“Tumejipanga kushinda tena licha ya kuwa tunacheza ugenini,” alisema Mgosi ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Simba.


Katika mechi ya mwisho, kwenye uwanja huo, Simba iliitandika Mwadui FC kwa mabao 3-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV